17 Juni 2016 - 23:10
 Riyadh Hadadi: Abubakari Al-Baghdadiy bado yuko hai

Balozi wa Syria mjini Moscow asema kuwa: hatuna habari za uhakika zinaonyesha kuwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh kwamba amekufa, pamoja kuwa tunafahamu kuwa amejeruhiwa na inshallah hivi karibuni ataangamia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: balozi wa Syria nchini Urusi ameashiria taarifa za kuangamia kwa  kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh “Abubakar Al-Baghdadiy” akisema: kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh bado yuko hai pamoja kuwa tunafahamu kuwa amejeruhiwa.
Riyadh Hadadi aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na shirika la habari la Urusi, akifafanua suala hilo alisema: hatuna ripoti za mashiko zinazothibitisha kuangamia kwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, ama tunafahamu kuwa kiongozi huyo amejeruhiwa, katika masiku yajayo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu yeye na viongozi wenzake wataangamia.
Baadhi ya vyombo vya habari siku ya Jumatatu iliopita vilitoa kauli inayohusishwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh kuwa kimetangaza kifo cha kiongozi wa kikundi hicho.
Vyombo hivyo vya habari vilitangaza kuwa kiongozi huyo ameangamia kufuatia mashambulizi ya anga yaliofanywa na ndege za makubaliano ya umoja wa mataifa wa kupambana na ugaidi ambapo siku ya Ijumaa alijeruhiwa na baadaye kufa na kuangamia. Ama mpaka sasa umoja huo haujathibitisha kuuwawa kwa kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
mwisho wa Habari/290